1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa uchumi wa Ujerumani na Asia Pazifik

5 Oktoba 2007

Huu ni mkutano wapili kufanyika huko Seoul.Biashara na eneo hilo inazidi kustawi huku Asia ikizidi kuwa gurudumu la ukuaji uchumi ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/C7s2

Waziri wa uchumi wa Ujerumani Bw.Michael Glos akiandamana na makamo-rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya,Günther Verheugen,wanafungua hii leo mjini Seoul,Korea ya Kusini, mkutano wa uchumi wa Ujerumani na nchi za Asia-Pazifik.

Zaidi ya 10% ya biashara ya nje ya Ujerumani,inafanywa na nchi za Asia. Biashara hii sasa inalengwa hata kuimarishwa zaidi na ndio shabaha ya mkutano unaofunguliwa leo mjini Seoul.

Mkutano huu ni wapili wa halmashauri ya Asia-pazifik ya viwanda vya Ujerumani nchini Korea ya kusini.Katika mkutano wa kwanza hapo 1992,wanaviwanda 120 wa kijerumani walishiriki.

Safari hii watakuwa 600 mio ngoni mwao mameneja maarufu wa hadhi ya juu.Mnamo miaka 15 iliopita sio tu nafasi ya Korea ya kusini katika uchumi wa dunia imeimarika zaidi, bali pia biashara na raslimali baina ya Ujerumani na Korea kusini imeongezeka mno.

Kwani, Korea ya kusini ambayo vizazi vichache tu nyuma iliokua nchi masikini,leo hii inasimama nafasi ya 12 miongoni mwa nchi zinazoongoza kiviwanda ulimwenguni.

Biashara kati ya Ujerumani na Korea imefikia dala bilioni 21 kwa mwaka tena yenye wezani ulio sawa kwa pande zote mbili.Raslimali ilizotia Ujerumani nchini Korea ya Kusini imefikia dala bilioni 7.5.Kwani, mbali na makampuni kama vile BASF,BAYER,BOSCH,ALLIANZ na Dt.Bank,zaidi ya viwanda 200 vya ukubwa wa wastani vya Ujerumani vimeekeza nchini Korea ya kusini.

Kwa jumla, viwanda hivyo vinawaajiri kiasi cha watumishi laki 1.

Bara la Asia ndilo gurudumu linalosukuma mbele uchumi wakati huu duniani.Kwa biashara yake ya nje,ile inayoagiza nchini kutoka nje na raslimali,viwanda vya Ujerumani vinachangia navyo katika kustawisha uchumi wa Kusini-mashariki mwa Asia.

Bw.Jürgen Hambrecht,mwenyekiti wa halmashauri ya uchumi ya Asia-Pazifik,anahisi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa huko na matatizo ya kimazingira kuna changamoto za kiufundi zinazobidi kukabiliwa ili kusimama wima katika soko la asia.Anasema,

“Hapa ni ufundi mpya ndio utakatusaidia kusonga mbele.Ufundi huo utumike kwa jicho la kuendeleza mafanikio ya kiuchumi yanayoselelea katika kila pembe ya dunia na hasa Asia.Naiona Ujerumani iko katika hali bora hapa.”

Swali linalozuka katika kikao hiki cha Seoul, ni jinsi gani ushirikiano huo wa kiufundi-mambo-leo unawezekana chini ya hali ya mashindano makali ya kibiashara.Kwani tayari 70% ya makampuni ya ujerumani yaliopo China yalalamika juu ya kuibiwa ufundi wao.Waziri wa uchumi wa Ujerumani Bw.Michael Glos hapa anasema:

“Kwa hali hii, viwanda vinapata hasara kubwa.

Na pana haja kubwa ya kuchukuliwa hatua na hata na wanasiasa kuirekebisha hali hii.Kupitia shirika la OECD tutazungumza na nchi zinazonyanyukia kiuchumi kwa lengo la kulinda haki-miliki.Tumo mfululizo tukiwasiliiana na China. Kwa kujiunga Chimna na Shirika la Biashara Duniani,imechukua jukumu la kulinda haki miliki….”

Kuimarika kwa nguvu za uchumi za bara la Asia,kumevifungulia milango ya nafasi mpya za biashara viwanda vya Ulaya.Mbali na hayo, nchi za Ulaya zinapaswa kufurahia kuwa mamilioni ya watu huko Asia wamfaulu kujikomboa kutoka balaa la umasikini na hawategemei tena ruzuku kutoka kwao.