1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Ulaya na Afrika kufunguwa uhusiano mpya

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYOB

BRUSSELS

Mkutano wa wiki hii wa viongozi wa Ulaya na Afrika utafunguwa awamu mpya ya uhusiano kati ya mabara hayo mawili licha ya kususiwa kwa mkutano huo na Waziri Mkuu wa Uingereza.

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Manuel Barroso amesema leo hii Afrika lazima ipewe kipau mbele katika uhusiano wao wa nje.Amesema wakati umefika wa kubadili kabisa misimamo inayoshikiliwa baina ya nchi na nchi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown anasusia mkutano huo wa mwishoni mwa juma mjini Lisbon Ureno kupinga kuhudhuria kwa Rais Robert Mugabe ambaye Umoja wa Ulaya unamtuhumu kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.