1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa umoja wa Ulaya kuhusu Ukimwi mjini Bremen.

Mohammed Abdul-Rahman12 Machi 2007

Mada kuu ni pamoja na njia za kudhibiti wimbi la virusi vya HIV , ulaya amashariki.

https://p.dw.com/p/CHIO
Waziri wa afya wa Ujerumani Ulla Schmidt.
Waziri wa afya wa Ujerumani Ulla Schmidt.Picha: AP

Vita vya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi, ni mada inayojadiliwa katika mkutano wa Umoja wa ulaya kuhusu janga hilo katika mji wa Ujerumani wa Bremen. Mkutano huo leo na kesho,unafanyika chini ya kauli mbiu “ Kuwajibika na ushirikiano wa pamoja dhidi ya Ukimwi.” Mkutano huo unahudhuriwa na wataalamu pamoja na mawaziri wa afya.

Ujerumani pekee kwa mujibu wa tarakimu za wizara ya afya ,kuna zaidi ya watu wapya 2.700 walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ukimwi. Duniani kote kuna kiasi ya watu 40 milioni walioambukizwa virusi vya ukimwi-HIV.

Vikilinganishwa na virusi vyenginevyo, virusi vya HIV ni vigeni zaidi, lakini tangu wakati huo virusi hivyo visivyokua na tiba vimezagaa katika nchi nyingi duniani.

Katika kutanabahisha juu ya hatari ya janga hili, Waziri wa afya wa Ujerumani bibi Ulla Schmidt ,“ Ukimwi sio tu tatizo la nchi za ulimwengu wa tatu pekee bali pia nchini Ujerumani linazidi kuwa kubwa.Kibaya zaidi ni kuwa idadi ya wanaoambukizwa ina zidi. Kwa hivyo hapana budi kuendelea kutanabahisha kwamba Ukimwi unauawa na unabakia kuwa ugonjwa unaouwa.”

Kwa mujibu wa wataalamu ni kwamba kila mwaka takriban watu milioni 5 wanaambukizwa virusi vya ukimwi HIV. Tangu janga hili lilipoanza, karibu watu 25 milioni walioambukizwa duniani kote wamefariki dunia. Nchini Ujerumani pekee mwaka jana walikufa watu 2.700 walioambukizwa ugonjwa huo.

Ugonjwa huu umegeuka kuwa tatizo kubawa kwa mataifa ya Afrika kusini mwa bara hilo na pia barani Asia. Tangu kuanguka kwa iliokua Urusi ya zamani, pia janga hili limelikumba eneo la mashariki mwa bara la Ulaya. Kwa mujibu wa mtaalamu wa virusi vya HIV Daktari Ulrich Markus kutoka taasisi ya Robert Koch, kwa miaka mingi sasa uambukizaji wa wa virusi hivyo umechangiwa pia na matumizi ya madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano, ambapo waathirika hutumia sindano zilizotumiwa na wengine.

Kutokana na hayo ulaya mashariki limeguka eneo linalopaswa kupewa zingatio kubwa katika mkutano huu wa nchi za umoja wa ulaya mjini Bremen. Miongoni mwa yanayopaswa kuzingatiwa kama sehemu ya hatua za kuudhibiti ugonjwa huo,kwa mujibu wa waziri Schmidt ni kwamba ,“Kwa mfano ni pendekezo la hatua maalum za kinga kwa watu ambao msingi wao ni wahamiaji au hata pendekezo la kinga kwa wanaosafiri kuelekea nchi ambazo kiwango cha uambukizaji ni kikubwa, kwa ushirikiano na sekta za utalii.”

Mkakati wa umoja wa mataifa ni kuhakikisha wimbi hili la uambukizaji Ukimwi kufikia 2015. Kutokana na hayo wiki iliopita serikali ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, ilitangaza kuongeza fedha vita dhidi ya Ukimwi. Hivyo kwa mwaka 2007 patatumika euro milioni 400 katika vita dhidi ya virusi vya HIV.

Leo na kesho, mawaziri wa afya wa umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuandaa mpango wa kuzuwia wimbi la uambukizaji linaloyakumba mataifa ya ulaya mashariki.