1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Umoja wa Ulaya na Bara Afrika mjini Lisbon

8 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZ1d

Takriban viongozi 80 kutoka Ulaya na Bara Afrika wamekusanyika Lisbon,Ureno kwa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Bara Afrika,ukiwa ni wa kwanza baada ya kipindi cha miaka saba.Mkutano huo wa siku mbili unaanza leo Jumamosi na unatazamia kuimarisha biashara na kuboresha ushirikiano katika sekta za uhamiaji na ulinzi wa amani.

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel na Rais wa Afrika Kusini,Thabo Mbeki watazungumza juu ya haki za binadamu na uongozi mzuri.