1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Umoja wa Ulaya na mataifa ya mashariki waaza

28 Novemba 2013

Maafisa wa Umoja wa Ulaya pamoja na Ukraine wamesema leo(28.11.2013) kuwa mazungumzo ya mahusiano ya karibu na nchi hiyo yanaweza bado kufufuliwa baada ya mkutano wa siku mbili unaoanza leo.

https://p.dw.com/p/1AQ82
European Union president Herman Van Rompuy (L) and European Commission president Jose Manuel Barroso give a press conference early on October 25, 2013 in Brussels. France and Germany pushed today for Washington to agree new rules on espionage after damaging revelations the United States tapped German Chancellor Angela Merkel's mobile phone and spied on other allies. Paris and Berlin will 'seek bilateral talks with the US' to reach an understanding by year's end on the conduct of intelligence gathering among allies, EU President Herman Van Rompuy told reporters after a first day of EU summit talks. AFP PHOTO / GEORGES GOBET (Photo credit should read GEORGES GOBET/AFP/Getty Images)
Van Rompuy (shoto) na Jose BarrosoPicha: Georges Gobet/AFP/Getty Images

Wakikabiliwa na mbinyo kutoka Urusi , viongozi wa Ukraine wiki iliyopita waliweka kando mipango ya kujiunga na Umoja wa Ulaya, hali iliyozusha maandamano makubwa ya umma nchini humo na kurejesha nyuma mipango ya Umoja wa Ulaya kulinyofoa taifa hilo lenye wakaazi milioni 46 kutoka himaya ya Urusi. Urusi inapendelea Ukraine ijiunge na umoja tofauti ambao una lengo la kushindana na Umoja wa Ulaya.

A deputy of the Ukrainian opposition reacts after voting in the parliament in Kiev on November 21, 2013.The Ukrainian parliament on Thursday voted against bills that would free jailed opposition leader Yulia Tymoshenko, dealing a potentially fatal blow to its chances of signing a historic trade deal with the EU at a summit this month. Watched by special EU envoys Aleksander Kwasniewski and Pax Cox, the Verkhovna Rada rejected all six bills that had been put forward on the treatment of convicts abroad after they failed to gain the support of President Viktor Yanukovych's ruling party. AFP PHOTO/SERGEI SUPINSKY (Photo credit should read SERGEI SUPINSKY/AFP/Getty Images)
Waandamanaji wakiwa na picha ya Julia TymoschenkoPicha: AFP/Getty Images

Utanuzi kuelekea mashariki

Makubaliano ya ushirika na Ukraine, kwa minajili ya kuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara, na Umoja wa Ulaya yalikuwa ni tukio la kutia saini baada ya mkutano huo wa siku mbili nchini Lithuania ambayo ni jamhuri ya zamani ya iliyokuwa Umoja wa Kisovieti, nchi ambayo hivi sasa ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, na ni ishara ya wazi kuwa Umoja huo unapanua ushawishi wake kwa njia ya kijiografia kuelekea zaidi upande wa mashariki, hadi katika mpaka na Urusi.

epa03948121 European Commission President Jose Manuel Barroso presents the European Semester Annual Growth Survey, Alert Mechanism Report and the employment and single market reports during a news conference at the EU headquarters in Brussels, Belgium, 13 November 2013. The Annual Growth Survey will set out general economic priorities for Member States to follow when drawing up their budgets and reform plans over the next year. The Alert Mechanism Report will screen EU economies for potential macroeconomic imbalances, and indicate which economies require further analysis. This year the Annual Growth Survey will be accompanied by the draft Joint Employment Report, which for the first time will include a scoreboard on employment and social policies, as well as a staff working document outlining how the country-specific recommendations have been implemented in the Member States. EPA/OLIVIER HOSLET pixel
Jose Manuel BarrosoPicha: picture-alliance/dpa

Badala yake kuanzisha rasmi mazungumzo ya makubaliano na jamhuri nyingine mbili za zamani za Umoja wa Kisovieti , mataifa ya Georgea na Moldova , yakiwa na wakaazi wapatao milioni 4.5 na 3.6, yatakuwa ni vivutio mbadala katika mkutano huo.

Pat Cox , rais wa zamani wa bunge la Umoja wa Ulaya ambaye hivi sasa anaongoza ujumbe wa uangalizi wa Umoja huo nchini Ukraine, amesema kuwa , "Ukraine , kama taifa huru, ina haki ya kusema 'ndio,' ' hapana' ama 'huenda' na kwa sasa inaonekana kuwa ni 'huenda'.

"Kuwapo kwangu hapa kuna maana kuwa tunaendelea kufanyakazi kwa pamoja, tuko tayari kukutana na kutafuta suluhisho," amesema Arbuzov , mshirika mkubwa wa rais wa Ukraine Viktor Yanukovych.

epa03151610 Ukraine's President Viktor Yanukovich is seen before posing for a family picture during the meetings of the EurAsEC Interstate Council and the Supreme Eurasian Economic Council in the Kremlin in Moscow, Russia 19 March 2012. The leaders of former Soviet republics, the Eurasian Economic Community (EurAsEC) member-states (Belarus, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Russia, Tajikistan) and observers (Armenia, Moldova, Ukraine), arrived to Moscow to discuss integration processes. EPA/YURI KOCHETKOV
Rais wa Ukraine Viktor JanukovichPicha: picture-alliance/dpa

Rais Yanukovich anatarajiwa kukutana na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya leo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo mjini Vilnius, ambako uhusiano kati ya pande hizo mbili uko mashakani. Halmashauri ya Umoja imesema kuwa rais wake , Jose Manuel Barroso atahudhuria mkutano huo pamoja na rais wa baraza la Ulaya Herman Van Rompuy, ambaye ndie atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre

Mhariri: Josephat Charo