1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa usalama wafunguliwa mjini Munich

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4yX

Beyrout:

Spika wa bunge la Libnan Nabih Berri ameakhirisha kwa mara nyengine tena kikao kilichopangwa kuitishwa jumatatu ijayo ili kumuidhinisha rais mpya.Nabih Berri amesema jaribio jipya la bunge litafanyika wiki mbili na nusu kutoka sasa.Hii ni mara ya 14 kwa kikao cha bunge kuakhirishwa kutokana na kutokuwepo maridhiano kati ya serikali ya muungano inayoungwa mkono na Marekani na upande wa upinzani unaoelemea upande wa Syria.Libnan haina rais tangu mhula wa Emile Lahoud ulipomalizika November 23 mwaka jana.