1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika wanamlizika.

Tuma Dandi3 Julai 2007

Washindwa kuafikiana juu ya kuundwa haraka Muungano wa mataifa ya bara hilo .Baadhi ya mataifa yamependekeza kuimarisha uchumi na ushirikiano wa kimataifa, na kutoka muda zaidi kwa maandalizi ya Muungano wa Afrika.

https://p.dw.com/p/CB36
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, aliyependekeza Muungano wa haraka.
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, aliyependekeza Muungano wa haraka.Picha: dpa - Report

Ndoto za kuundwa kwa muungano wa Afrika zimefikia tamati baada ya viongozi kadhaa kuonesha wazi kwamba si wakati muafaka wa kuunganisha nchi zote pamoja.

Nchi za kusini na Mashariki mwa afrika zimeonesha kwamba wazo la kuifanya Afrika kuwa moja haliwezekani kwa sasa, badala yake muda zaidi utolewe kwa ajili ya maandalizi.

Katika kuhitimisha mjadala huo katika kilele cha mkutano wa AU mjini Accra nchini Ghana muda mfupi uliopita, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametoa wazo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya uchumi na biashara miongoni mwa nchi wanachama.

Rais Museveni amesema ni vema kufanya mahusiano na watu wa jamii moja katika mambo yanayofanana.

Aidha, rais mpya wa Nigeria Bwana UMARU YAR’ ADUA, amesema pamoja na lengo hilo kuwa zuri kwa manufaa ya waafrika, ni vema kila nchi ikawajibika katika uhusiano kabla ya kuingia katika Muungano.

AU imebaki katika mgawanyiko, huku viongozi wenye msimamo kamili wakiongozwa na Rais Muammar Gaddafi wa Libya na Abdoulaye Wade wa Senegal, wakihakikisha kwamba wazo hilo halitofutika vichwani mwao.

Wana ndoto za kuona Afrika yenye mshikamo ikiwa na jeshi la pamoja, uchumi wa pamoja, mahusiano kati ya nchi na nchi na baadaye Muungano kamili.

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal amezitaka nchi za magharibi mwa afrika kuanza ushirikiano wa pamoja, ili baadaye mataifa mengine yaweze kusaini mkataba wa umoja.

Akiongoza taifa linalofuata mfumo halisi wa kidemokraisa, rais huyo amesema huenda Afrika Magharibi ikianza kusaini mkataba huo, nchi zingine za Afrika zitafuata.

Waziri wa mambo ya nje wa Ghana Bwana NANA AKUFO-ADO amesema walitarajia kuona mgawanyiko huo, lakini akasema nchi yake inaamini kwamba kila kitu kina wakati wake, na kwamba kuungana kunawezekana.

Msimamo wa viongozi wa AU ni kuona nchi zao zikiwa na uchumi mzuri, demokrasia na ushirikiano wa kimataifa, ndipo wakubali kusaini mkataba wa Muungano wa Afrika.