1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza kujengwa upya, nani apewe fedha?

Abdu Said Mtullya2 Machi 2009

Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 70 wanahudhuria mkutano wa wafadhili nchini Misri kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/H410
Wafadhili wajadili mpango wa kuujenga upya Ukanda wa Gaza.Picha: Bettina Marx

Wajumbe kutoka nchi zaidi ya70 wanakutana Scharm el-Sheikh kujadili mpango wa kuujenga upya Ukanda wa Gaza.

Hatahivyo wafadhili wanakabiliwa na swali muhimu. Ni nani anaestahili kupewa fedha kwa ajili ya ujenzi huo mpya.?

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo wa wafadhili wa kimataifa ,unaofanyika kwenye kitongoji cha Sharm al- Sheikh nchini Misri, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua mara moja.Amesema lazima ujenzi mpya uanze mara moja na amani ya kudumu irejeshwe baina ya Israel na wapalestina.Ametamka kuwa watu wa Gaza hawawezi kuendelea kusubiri.

Katika juhudi za kuujenga upya Ukanda wa Gaza , nchi za Umoja wa Ulaya zimeahidi kutenga Euro nusu bilioni. Marekani imesema itatenga dola milioni 900 na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier anaratajiwa kuahidi mchango wa Euro milioni 100.

Lakini wafadhili wanakabiliwa na swali muhimu-ni nani anaestahili kupewa fedha hizo kwa ajili ya kuijenga upya Gaza.

Akizungumza kwenye mkutano huo wa Sharm al-Sheikh ,rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema serikali yake imefafanua mpango wa kuujenga upya Ukanda wa Gaza utakaoinua uchumi wa sehemu hiyo.Bwana Abbas ameeleza kuwa wapalestina hawana njia nyingine ili kukubliana kufikia maridhiano.Ametamka kuwa wapalestina wapo tayari kumaliza tofauti zao na kutangaza serikali ya umoja ili kuweza kutayarisha uchaguzi mkuu mwezi januari mwaka ujao.

Hatahiyvo msemaji wa Hamas Fawzi Barhum ametoa mwito juu ya kujengwa upya kwa Ukanda wa Gaza lakini ameitaka jumuiya ya kimataifa isiegemee upande wowote.

Israel,Marekani na Umoja wa Ulaya zimesema msaada utakaotolewa lazima upitishiwe kwa mamlaka ya Palestina ya rais Mahmoud Abbas anaeungwa mkono na nchi za magharibi.