1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Platini anastahili kumrithi Blatter

10 Julai 2015

Herbert anasema Platini ndiye mgombea bora kwa sababu analiongoza Shirikisho la Kandanda Ulaya – UEFA iliyo na vilabu imara na dimba maarufu na bora kabisa la Champions League

https://p.dw.com/p/1Fwcx
Herbert Hainer
Picha: picture-alliance/dpa

.Anaongeza kuwa Mfaransa huyo amefanya kazi nzuri katika mihula yake miwili aliyokuwa uongozini. Adidas ni mfadhili mkuu wa mchezo wa kandanda. Herbert anasema ikiwa Platini ataamua kugombea urais wa FIFA, mkuu wa SHirikisho la Kandanda la Ujerumani – DFB Wolfgang Niersbach anaweza kugombea nafasi ya kumrithi katika shirikisho la UEFA.

Platini aliamua kutogombea dhidi ya Blatter katika uchaguzi wa FIFA lakini huenda akawa mgombea sasa. Amekuwa mkuu wa UEFA tangu 2007 na alichaguliwa kuongoza kwa muhula wa tatu mapema mwaka huu. Niersbach ni mwanachama wa kamati kuu za UEFA na FIFA.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman