1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa al-Qaeda Afrika Mashariki ameuawa

12 Juni 2011

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton, amesifu taarifa za kifo cha mkuu wa wanamgambo wa al-Qaeda, Fazul Abdullah Mohammed

https://p.dw.com/p/11Ys4
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary ClintonPicha: AP

Waziri Clinton, alipozungumza na waandishi wa habari akiwa ziarani nchini Tanzania, alisema kifo cha Fazul Abdullah ni " pigo kubwa" kwa al-Qaeda na washirika wake katika eneo la Afrika Mashariki.

Fazul Abdullah Mohammed
Fazul Abdullah MohammedPicha: picture-alliance/dpa

Fazul aliekuwa akitazamwa kama kiongozi wa al-Qaeda katika eneo la Afrika Mashariki, aliuawa jumanne iliyopita mjini Mogadishu. Fazul aliekuwa na umri wa miaka 38, alikuwa akisakwa kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998, yaliyosababisha vifo vya watu 224.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Prema Martin