1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa IMF azuilwa na polisi

15 Mei 2011

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Dominique Strauss-Kahn, ameshikiliwa na polisi jijini New York akihojiwa kwa tuhuma za shambulio la aibu dhidi ya mhudumu wa kike katika hoteli moja jijini humo.

https://p.dw.com/p/RNz9
International Monetary Fund (IMF) Managing Director Dominique Strauss-Kahn takes part in the opening news conference for the annual IMF and World Bank meetings, Thursday, Oct. 7, 2010, in Washington. (AP Photo/Haraz N. Gha
Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Dominique Strauss-KahnPicha: AP

Hapo awali, polisi ilimtoa Strauss-Kahn kutoka ndege aliyokuwa amepanda kuelekea Paris, Ufaransa, akiwa kwenye uwanja wa ndege wa John. F. Kennedy, jijini New York.

Strauss-Kahn, ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa, anaonekana kama miongoni mwa wagombea wa urais wa Ufaransa katika uchaguzi wa mwakani.