1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa majeshi ya Ujerumani ajiuzulu

Aboubakary Jumaa Liongo26 Novemba 2009

Mkuu wa jeshi la Ujerumani, Wolfgang Schneiderhan, amejiuzulu.

https://p.dw.com/p/Kglc
Mkuu wa majeshi ya Ujerumani Jenerali Wolfgang SchneiderhanPicha: picture-alliance/ dpa

Akitoa taarifa hiyo bungeni Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg, alisema Bwana Schneiderhan ameomba mwenyewe kuacha kazi.

Kamanda Schneiderhan amechukuwa uamuzi huo kutokana na lawama kwamba wizara ya ulinzi ilizuwi kutoa maelezo kwa wananchi na kwa mwendesha mkuu wa mashtaka kuhusu raia waliouawa kwa shambulio la ndege liloamriwa kufanywa na jeshi la Ujerumani mwanzoni mwa mwezi Septemba nchini Afghanistan.Shambulio hilo lililengwa dhidi ya malori ya mafuta.

Hapo kabla, waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, alishikilia kurefushwa muda wa kuyabakisha majeshi ya Ujerumani katika Afghanistan, na, wakati huo huo, akatangaza kwamba serikali itakuwa wazi na itasema ukweli juu ya shughuli za jeshi hilo.

Serekali itarefusha muda wa jeshi hilo kuweko Afghanistan kwa mwaka mmoja hadi mwisho wa mwaka 2010. Idadi ya wanajeshi hao 4,500 itabakia hivyo hivyo , bila ya kubadilika.

Lakini kwa mujibu wa Gazeti linalochapishwa mjini Cologne , Kölner Stadt-Anzeiger, wizara ya ulinzi inafikiria kuongeza idadi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan kufikia 6,500.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Abdul-Rahman