1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlinzi ahojiwa kifo cha Okende

20 Julai 2023

Mlinzi wa mwanasiasa wa upinzani aliyepatikana amefariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni miongoni mwa watu kadhaa wanaohojiwa na wachunguzi.

https://p.dw.com/p/4UA9p
Demokratische Republik Kongo Kinshasa | Cherubin Okende
Cherubin Okende, waziri wa zamani wa usafirishaji na baadae kuhamia upinzani aliuawa Julai 13, 2023.Picha: Samy Ntumba Shambuyi/AP/picture alliance

Hayo ni kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Kinshasa inayosimamia uchunguzi kuhusu mauaji ya Cherubin Okende.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Firmin Mvonde, amewaambia waandishi wa habari kwamba mlinzi huyo ambaye aliwekwa kizuizini siku hiyo hiyo amekuwa akitoa kauli zinazokinzana na kuongeza kuwa dereva wa Okende na watu wengine bado wanahojiwa.

Okende, aliyekuwa waziri wa zamani wa uchukuzi mwenye umri wa miaka 61, alikutwa amefariki katika gari lake Julai 13 huku mwili wake ukiwa na majeraha ya risasi.

Alikuwa pia kada wa chama kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo cha Ensemble Pour la Republique cha Moise Katumbi ambaye anatazamiwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Disemba mwaka huu.