1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuaji wa kujitolea mhanga ajilipua Yemen

21 Mei 2012

Mlipuaji wa kujitolea mhanga amejilipua na kusababisha vifo vya wanajeshi mamia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya mapema leo nchini Yemen wakati wa mazoezi maalumu ya kuadhimisha miaka 22 ya Muungano wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/14zHV
Mlipuko wa Yemen
Mlipuko wa YemeniPicha: Reuters

Mlipuaji huyo akiwa amevalia mavazi rasmi kama askari wa Yemen alijiingiza katika kikosi cha wanajeshi hao na kujiripua na kusababisha vifo vya askari hao na majeruhi kadhaa ambao waliokuwemo katika mazoezi hayo ya gwaride la maadhimisho.

Majeruhi hao walionekana wakibebwa na teksi kupelekwa kupatiwa matibabu na kuna kila dalili za waliofariki kuongezeka kwani mashuhuda wameona viungo vya miili ya binadamu vikiwa vimetapakaa katika uwanja wa Al- Sabeen.

Mazoezi haya maalumu ya kuadhimisha miaka 22 ya muungano baina ya Yemeni ya Kaskazini na Kusini yakishuhudiwa na Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi ya Yemen ambao hawakupata majeraha yoyote. Maadhimisho haya yalikuwa ni ya kujiandaa na maadhimisho ya muungano ambaye yamepangwa kufanyika Jumanne.

Sanaa
SanaaPicha: Reuters

Kama ilivyodesturi ya mazoezi hayo kufanyika kila mwaka kabla ya maadhimisho yake kufanyika ambapo maadhimisho haya ya muungamo hufanyika na kuwahusisha wanajeshi wengi pamoja na vikosi vingine vya ulinzi na usalama vya taifa hilo.

Tukio hili ni miongoni mwa tukio kubwa kuwahi kuikumba Yemen tangu kuingia madarakani kwa Rais Abdrabuh Mansur mwezi February mwaka huu na kuweka wazi atapambana na ugaidi na hasa akilinyooshea kidole kundi la Al-Qaeda ambalo limeonekana kuweka mizizi nchini humo na kuenea kwa kasi.

Shambulio hili linatokea siku ya kumi sasa baada ya Jeshi la Yemen kuwashambulia wanamgambo wa Al-Quada katika jimbo la Kusini la Abyamn. Pia wachunguzi wa masuala ya ulinzi na usalama wanaona kuwa tukio hilo si hatari kwa Yemen tu bali kwa Marekani pia.

Muungano wa Yemen wa Mei 22,1990

Maadhimisho hayo ambayo yanafanyika tarehe 22 Mei yatahudhuriwa na Rais Abd Rabbu Mansour Had. Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi iliyotolewa juu ya tukio hilo huku watoa taarifa kutoka vikosi ya usalama vya Yemen wakiomba kutokujukana.

Wanajeshi wa Yemen
Wanajeshi wa YemenPicha: Reuters

Maadhimisho haya ya Muungano wa Yemen uliofanyika tarehe 22. Mei mwaka1990 na kuunda Jamhuri ya Yemen ni ya kwanza tangu kukubali kujiuzulu kwa Rais Ali Abdullah Saleh baada ya makubaliano ya Novemba yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa baada ya kufanyika maandamano ya kuupinga utawala wake. Hali hiyo ikafanya uchaguzi kufanyika na Februari mwaka huu na Rais Abd Rabu Mansour akawa Rais waYemen.

Mwandishi :Adeladius Makwega/AFP/RTRE/DPAE

Mhariri Yusuf Saumu

.