1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuko wa bomu wauwa watano.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkEE

Ankara.

Maafisa nchini Uturuki wanasema kuwa kiasi watu watano wameuwawa na zaidi ya 60 wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika eneo la Diyarbakir, mji mkubwa kabisa katika eneo la Wakurdi wa Uturuki upande wa kusini mashariki. Mlipuko huo unaripotiwa kuwa umetokea wakati gari la jeshi lilipokuwa linapita katika barabara katikati ya mji huo. Mji huo unaidadi kubwa ya wanajeshi ambao wanapambana na waasi wa kundi la PKK ndani ya Uturuki na katika nchi jirani ya Iraq. Ripoti ambazo hazikuthibitishwa zinasema kuwa shambulio hilo la bomu huenda ni kulipiza kisasi kwa waasi wa PKK dhidi ya mashambulizi ya ndege za kijeshi za Uturuki katika maeneo ya waasi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq mwezi uliopita.