1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuko watokea jijini Nairobi

11 Juni 2007

Mlipuko wa bomu umetokea leo asubuhi katikati ya jiji la Nairobi nchini Kenya mtu wawili wameuwawa na wengine 30wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/CB3h
Mahali pa mlipuko jijini Nairobi
Mahali pa mlipuko jijini NairobiPicha: AP
Chanzo cha mlipuko bado hakijajulikana ila kwa mujibu wa Kamishna wa polisi Mohamed Hussein Ali mlipuko ulisababishwa na kitu kilichobebwa na mtu.

Polisi wanaeleza kuwa uchunguzi wa kwanza unabaini kuwa mtu mmoja alijaribu kuingia mkahawa mmoja nao walinzi walijaribu kumzuia kuingia kwani alikuwa na mavazi ya kutatanisha. Haijulikani iwapo mtu huyo alihusika na mlipuko huo.Mlipuko huo umetokea kwenye duka moja katika Hoteli ya Ambassadeur. Hoteli yenyewe haikuathirika.