1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHOU:Mapambano yapambamoto nchini Somalia

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDY

Mapambano makali yameingia katika siku ya tatu mjini Mogadishu ambapo majeshi ya Ethiopia yanapambana vikali na wapiganaji wa kiislamu. Mapigano yalishtadi baada ya helikopta ya Ethiopia kuangushwa na wapiganaji wa kiislamu. Wanajeshi wawili waliokuwamo katika ndege hiyo waliuawa.

Serikali ya Ethiopia imesema majeshi yake yalijibu shambulio hilo kwa kuwaua waasi 200.