1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHOU.Watu zaidi wauawa Mogadishou

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC88

Watu zaidi ya 60 wameuawa katika siku ya nne ya mapigano makali baina ya majeshi ya Ethiopia na wanamgambo wa kiislamu. katika mji mkuu wa Somalia Mogadishou.

Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya laki tatu wameshaukimbia mji huo tokea mwezi wa februari kutokana na mapigano.

Hadi sasa watu zaidi ya 130 wameshauawa kutokana na mapigano na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika siku za karibuni.

Majeshi ya Ethiopia yaliingia katika mji wa Mogadishu mwezi desemba ili kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia kuwakabili wapiganaji wa mabaraza ya kiislamu.