1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Amri ya hali ya hatari kutumika nchini Somalia.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCap

Bunge la Somalia limepiga kura likikubali sheria ya kijeshi kutumika nchini humo na kuiruhusu serikali ya mpito kuweka sheria ya hali ya hatari kwa muda wa miezi mitatu.

Naibu spika wa bunge amesema kuwa wabunge 154 walipiga kura ya kukubali hoja hiyo, wakati wabunge wawili walipinga.

Hii inakuja wakati majeshi ya serikali , yakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia, yamesema kuwa yamelikamata eneo la mwisho lililokuwa ngome ya wapiganaji wa Kiislamu katika eneo la kusini nchini humo.

Msemaji wa serikali amesema kuwa jeshi hilo limechukua kijiji kilichoko pwani cha Ras Kamboni ambako wapiganaji hao wa Kiislamu wakiwa wanakimbia walijificha.