1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Gedi anusurika tena kuuwawa

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1F

Waziri Mkuu wa Somalia Ali Mohamed Gedi ameepuka kuuwawa baada ya msafara wake kukanyaga bomu lililotegwa ardhini ambalo limeshindwa kuripuka kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Gedi alikuwa akirudi kutoka uwanja wa ndege mkuu wa mji huo katika shuguli za kusindikiza maiti za wanajeshi wanne wa kulinda amani wa kikosi cha Umoja wa Afrika kutoka Uganda waliouwawa hapo juzi.

Kwa mujibu wa afisa kutoka ofisi ya Gedi bomu hilo liliwacha moshi mkubwa baada ya kushindwa kuripuka.Mashahidi wanasema maafisa wa waziri mkuu waliruka kutoka kwenye magari yao na kufyetuwa risasi hewani baada ya kukanyaga bomu hilo.

Hakuna mtu aliejeruhiwa katika tukio hilo katika kitongoji cha Juba kaskazini mwa Mogadishu likiwa ni jaribio la tatu la tishio la maisha ya Gedi tokea alipochaguliwa kuongoza serikali ya Somalia hapo mwaka 2004.