1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Hali inageuka maafa ya kibinaadamu

25 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7P

Mashirika ya misaada ya kimataifa yanasema hali katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu inageuka kuwa maafa ya kibinaadamu.

Maelfu kwa maelfu ya watu waliokuwa wakihitaji mno maji safi ya kunywa na chakula wamekimbia mapigano mapya kati ya vikosi vya Somalia vikiungwa mkono na vya Ethiopia na waasi wa Kiislam.Kundi la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka limesema kipindupindu na magonjwa mengine yameenea kwenye makambi ya kujishikiza yaliowekwa kuhifadhi wakimbizi.

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema mapigano mjini Mogadishu ni mojawapo ya mapigano mabaya kabisa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 16. Kikosi cha Umoja wa Afrika cha wanajeshi 1,500 wa Uganda kimeshindwa kuzuwiya umwagaji damu nchini Somalia na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya zinataka kikosi kikubwa zaidi cha Umoja wa Afrika kuchukuwa nafasi ya kikosi cha Ethiopia nchini humo.

Zaidi ya watu 200 wameuwawa kutokana na mapigano wiki iliopita.