1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Helikopta imeshambulia ngome ya waasi

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEX

Mapigano mapya yamezuka katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu.Kwa mujibu wa ripoti za waandishi wa habari,helikopta ya jeshi la Ethiopia,ilishambulia ngome ya waasi na watu wengi wameuawa.Inasemekana mapigano kati ya vikosi vya Kiethiopia na waasi wasiojulikana yalizuka kusini mwa mji wa Mogadishu.Wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu waliotimuliwa na vikosi vya serikali ya Somalia na Ethiopia,wanalaumiwa kuhusika na machafuko ya umwagaji damu katika mji huo mkuu.Umoja wa Afrika umepeleka wanajeshi 1,200 kusaidia kuleta amani nchini humo,lakini hata vikosi hivyo vinashambuliwa.Juma lililopita si chini ya watu 30 waliuawa katika mapigano yaliyozuka kati ya waasi na wanajeshi wa Somalia na Ethiopia.