1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Kamanda ataka wanajeshi zaidi.

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGx

Kamanda wa majeshi ya umoja wa Afrika yanayolinda amani nchini Somalia ametoa wito jana wa kupatiwa wanajeshi zaidi , wakati mkuu wa usalama wa umoja wa Afrika alipofanya ziara katika mji mkuu wa Mogadishu.

Meja Jenerali Levy Karuhanga kutoka Uganda alitoa wito wa kupatiwa wanajeshi zaidi baada ya kukutana na mkuu wa masuala ya usalama wa umoja wa Afrika Said Djinnit, ambaye alikuwa mjini Mogadishu kwa ziara ya siku moja chini ya ulinzi mkali.

Karuhanga ambaye hivi sasa ana wanajeshi 1,500 kutoka Uganda , alikuwa akizungumza wakati watu wenye silaha walipolipua bomu kando ya barabara na kuushambulia mlolongo wa magari ya umoja wa mataifa ambayo yalikuwa yakielekea mjini Mogadishu.