1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Kituo cha televisheni cha Al Jazeera na redio tatu zafungiwa

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaM

Serikali ya mpito ya Somalia imeamuru kituo cha televisheni cha Al Jazeera kinachomilikiwa na Qatar na vituo vitatu vya redio vya Somalia vikome kurusha matangazo kutoka mjini Mogadishu.

Katika barua yake kwa vituo hivyo serikali ya Somalia imeviamuru vikomeshe kazi zao mara moja na viongozi wao waripoti kwa makao makuu ya shirika la ujasusi la taifa hapo kesho wapewe maelezo zaidi kuhusu uamuzi huo. Redio za Somalia zilizofungiwa ni Radio Shabele, Radio HornAfrik na Sauti ya Quran.

Wakati haya yakiarifiwa, watu watatu wameuwawa leo mjini Mogadishu katika mapigano makali kuwahi kutokea tangu wanamgambo wa mahakama za kiislamu walipofurushwa kutoka mjini humo.

Watu wawili wameuwawa kwenye mapigano kati ya vikosi vya usalama na waasi kwenye ngome ya waasi kusini mwa Mogadishu. Mtu wa tatu aliyeuwawa kwa kupigwa risasi ni afisa wa polisi aliyeshambuliwa na genge la waasi alipokuwa akilinda shehena ya silaha.