1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Maafa ya kibinaadamu yanyemelea Somalia

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8z

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ameonya juu ya maafa ya kibinaadamu nchini Somalia kama matokeo ya kuongezeka kwa umwagaji damu na kushindwa kupata msaada wa faraja kwa wale wanaouhitaji.

Eric Laroche mratibu wa misaada ya kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia amesema takriban watu 1,000 wanaojaribu kukimbia mapigano mjini Mogadishu wanahitaji sana maji na chakula.Wengi inasemekana wamekumbwa na tumbo la kuhara na kipindupindu.

Laroche amesema vikosi vya serikali ya Somali ambavyo vinapambana na waasi wa Kiislam vimekuwa vikizuwiya kufikishwa kwa msaada kwa maelfu ya watu waliopoteza makaazi yao.

Mapambano ya hivi karibuni kabisa yameuwa watu 12 na mwishoni mwa mwezi uliopita takriban watu 1,000 walikufa katika mapigano ya siku ya nne.