1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Maafa ya kiutu yakaribia Somalia.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8f

Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, linaonya kuwa maafa ya kiutu yanakaribia nchini Somalia , hususan katika mji mkuu Mogadishu.

Shirika hilo la kuwahudumia wakimbizi linakadiria kuwa zaidi ya Wasomali 200,000 wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano makali mjini Mogadishu na kwamba hali hiyo inaendelea.

Wakati mapigano hayo yanaendelea mjini Mogadishu rais wa serikali ya mpito Abdullahi Yusuf amesema kuwa mapigano hayo hayakuwa makubwa, ambapo wakaazi wa mji huo wanasema kuwa yameuwa watu 30 na kuwajeruhi wengine kadha.

Mwezi Desemba , majeshi ya Ethiopia yaliitimua serikali ya Kiislamu kutoka madarakani lakini mapigano yameanza tena katika wiki za hivi karibuni yakipambanisha kati ya wapiganaji na wanajeshi wa kiukoo kwa upande mmoja na majeshi ya Ethiopia na yale ya serikali ya mpito kwa upande mwingine.