1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Mabomu yauwa watu watatu

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCT0

Mabomu matano yaliovurumishwa na mizinga yameripuka kaskazini mwa Mogadishu leo hii na kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine kadhaa.

Katika umgwaji damu mpya kabisa baada ya kipindi cha vita kwenye mji mkuu huo wa Somalia wapiganaji wenye silaha katika sehemu mbali mbali wamekuwa wakivurumisha maroketi na kupelekea mapambano ya mizinga na wanajeshi wa serikali.

Madarzeni ya watu wameuwawa kutokana na mashmbulizi ya aina hiyo ambayo yamekuwa yakipamba moto tokea wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia wakisaidiwa na wale wa Ethiopia kuwatimua watawala wa Muungano wa Mahkama za Kiislam mwezi uliopita.

Mashambulizi hayo ya Mogadishu yamekuja masaa machache baada ya bomu kuripuka katika bandari ya Kismayo kusini mwa nchi hiyo ilioko kama kilomiata 500 kusini mwa mji wa Mogadishu ambapo watu wanne wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.