1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Maelfu ya wasomali waandamana kuipinga Ethiopia

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyg

Maelfu ya wasomali leo walijitokeza barabarani kufuatia mwito uliotolewa na viongozi wa mahakama za kiislamu waipinge hatua ya Ethiopia kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia ambayo haina nguvu. Katika miji na vijiji waandamanaji walichoma bendera za Ethiopia.

Maandamano ya leo yametumiwa pia kuwasajili wapiganaji zaidi watakaoshiriki katika vita vitakatifu vya jihad dhidi ya Ethiopia, nchi hasimu tangu jadi. Aliyeandaa maandamano ya mjini Mogadishu, Ahmed Qare, amewaambia waandamanji takriban elfu 15 kwamba wamepewa nafasi ya kushiriki katika vita dhidi ya adui aliyeivamia dini na nchi yao.

Kiongozi mwengine wa mahakama za kiislamu katika mji mwingine nchini Somalia amewaambia waandamanaji 1,200 kuwa mtu mmoja katika kila jamii anatakiwa kujiandikisha kama mpiganaji katika vita hivyo dhidi ya Ethiopia.