1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Maiti za wanajeshi zabururwa mitaani

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C78r

Nchini Somalia,kwa mara nyingine tena maiti za wanajeshi wa Kiethiopia zimebururwa na kutupiwa mawe katika mitaa ya mji mkuu Mogadishu. Wanajeshi hao waliuawa katika mapigano yaliyozuka upya kati ya vikosi vya Ethiopia na wanamgambo wa makundi ya Kiislamu kaskazini mwa Mogadishu.

Hapo kabla mamia ya waandamanaji walitoa mwito wa kuipindua serikali na kuvitaka vikosi vya kigeni kuondoka Somalia.Hadi wanajeshi 5 wa Ethiopia na raia 7 waliuawa siku ya Alkhamisi.Vikosi vya Ethiopia vinatoa msaada kwa serikali ya mpito ya Somalia.