1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Majeshi ya serikali yavamia mji mkuu.

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfS

Nchini Somalia , majeshi ya serikali yakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia yanakaribia kuuteka mji mkuu Mogadishu. Wapiganaji wanaounga mkono mahakama za Kiislamu wameondoka kutoka katika mji huo, wakisema kuwa wamefanya hivyo ili kuepusha uwagikaji wa damu.

Msemaji wa serikali ya muda ya Somalia aliwaambia waandishi wa habari kuwa hali ya hatari imetangazwa, yenye lengo la kurejea hali ya utulivu.

Mapigano yamezuka wiki iliyopita baada ya majeshi ya Ethiopia kupuuzia madai ya Waislamu ya kuondoa majeshi yao kutoka Somalia.

Wakati huo huo, baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa mara nyingine limeshindwa kukubali juu ya taarifa inayotoa wito wa kumalizwa kwa haraka kwa mapigano. Duru ya pili ya mazungumzo yalivunjika kutokana na sisitozo la Qatar kwamba taarifa hiyo iyatake majeshi ya Ethiopia na mengine ya kigeni kuondoka katika ardhi ya Somalia.