1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Makombora yameshambulia uwanja wa ndege

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLe

Mapigano makali yamezuka katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu muda mfupi baada ya uwanja wa ndege wa kimataifa mjini humo kushambuliwa kwa mizinga.Shambulio hilo lilitokea wakati ambapo baadhi ya vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika, kutoka Uganda viliwasili kwenye uwanja huo wa ndege.Wanamgambo walifyatuliana risasi na vikosi vya Somalia na washirika wake wa Ethiopia kwa takriban saa nzima.Wanajeshi wa Uganda ni sehemu ya vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika.Vikosi hivyo vimeidhinishwa na Umoja wa Mataifa kuilinda serikali ya mpito ya Somalia na kutoa nafasi kwa majeshi ya Ethiopia kuondoka nchini humo.Mwaka jana,majeshi hayo ya Ethiopia yalisaidia kuwashinda wanamgambo wa Kiislamu nchini Somalia.