1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Mapigano bado yanaendelea.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6o

Kumekuwa na mapigano zaidi mjini Mogadishu wakati majeshi ya Ethiopia yakiisaidia serikali ya mpito ya Somalia yalishambulia maeneo ya waasi wa Kiislamu wanaosaidiwa na wanamgambo wa kiukoo katika eneo la kaskazini ya mji huo.

Waziri mkuu wa Somalia Ali Mohammed Gedi amedai kuwa majeshi ya serikali yanashinda.

Wanadiplomasia wa magharibi , wakizungumza bila kutaka kutajwa majina , wamesema kuwa waasi wamepata hasara kubwa lakini hawajashindwa.

Umoja wa mataifa umeishutumu serikali ya Somalia kwa kuwanyima makundi ya kutoa misaada nafasi ya kuwafikia mamia kwa maelfu ya watu wanaokimbia , ambao wako katika makambi ya muda nje ya mji wa Mogadishu.

Mratibu wa misaada ya kiutu wa umoja wa mataifa John Holmes , akizungumza mjini Geneva , amezishutumu pande zote mbili kwa kuvunja haki za binadamu kwa kushambulia katika maeneo ya kiraia mjini Mogadishu.