1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu: Mapigano makali mjini Mogadishu.

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Br

IMapigano makali yamezuka tangu jana katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, baina ya majeshi ya Ethiopia na waasi wa Kisomali. Mashahidi wanasema si chini ya watu 10 wameuliwa kutokana na mashambulio ya makombora na mashinegani pale majeshi ya Ethiopia yalipofanya hujuma. Somalia imekuwa katika michafuko tangu pale serekali inayoungwa mkono na Ethiopia iwaondoshe madarakani watu wenye siasa za itikadi kali za Kiislamu. Mamia ya raia wameuwawa katika mapigano.