1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Mapigano makali yazuka tena.

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBK7

Kiasi cha watu 80 wameuwawa katika mapigano makubwa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, katika muda wa saa 48 zilizopita. Watu walioshuhudia pamoja na madaktari wamesema kuwa siku moja baada ya mashambulizi makubwa ya makombora na risasi yamesababisha vifo vya watu 50, na miili mingine mingi iligunduliwa kusini mwa mji huo.

Eneo hilo ndio jeshi la Ethiopia linalounga mkono serikali ya mpito ya Somalia imekuwa ikipambana na wapiganaji wa Kiislamu katika muda wa siku mbili zilizopita. Mapigano hayo yanaripotiwa kuwa makubwa sana katika mji huo tangu mwezi wa Aprili. Mamia ya raia wanasemekana kuwa wanakimbia mapigano hayo.