1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mapigano mapya yazuka mjini Mogadishu, Somalia

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZO
Rais Nicolas Sarkozy na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi
Rais Nicolas Sarkozy na kiongozi wa Libya Muammar GaddafiPicha: AP

Mapigano yamezuka upya nchini Somalia baada ya wanamgambo wasiojulikana kushambulia msafara wa majeshi ya Ethiopia, mjini Mogadishu.

Kiasi watu wawili wamearifiwa kuuawa.

Mapema, majeshi ya serikali yalizima shambulio dhidi ya makao ya rais wa muda, Abdullahi Yusuf mjini humo.

Wakati huo huo, Umoja wa Afrika umeidhinisha mpango wa kupeleka kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia ili kurejesha utangamano nchini humo.

Afisa mkuu wa Umoja huo amesema kikosi hicho kitapelekwa nchini humo kwa muda wa miezi sita na hatimaye kitasimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi hao watachukua nafasi ya wanajeshi wa Ethiopia waliokwenda nchini humo mwezi uliopita kuisaidia serikali ya mpito kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu.