1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Mapigano mapya yazuka.

1 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBdI

Kiasi watu 11 wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mapigano mapya nchini Somalia jana Jumanne, wakati wanamgambo wa Kiislamu wanaendelea na kampeni yao matumizi ya nguvu dhidi ya serikali ya nchi hiyo na washirika wake wa Ethiopia licha ya mkutano unaoendelea wa maridhiano.

Msemaji wa polisi amesema kuwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu bomu lililolipuka katika eneo la ufukwe wa bahari limeuwa kiasi raia watano. Ripoti za hapo awali zilisema kuwa mlipuko huo ulisababishwa na chombo kilichofyatuliwa kwa mbali.

Nje ya mji huo wanajeshi wanne wa Ethiopia wameuwawa baada ya kituo chao kushambuliwa na makombora na risasi kutoka kwa wanamgambo hao wa Kiislamu, ambapo miili ya wahanga wengine wawili ilipatikana katika jalala nyakati za asubuhi.