1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Mapigano yauwa watu wanane

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPC

Takriban watu wanane wameuwawa kusini mwa Mogadishu hapo jana baada ya kunaswa katika mapambano makali kati ya wanajeshi wa Ethiopia na wapiganaji wenye silaha wasiojulikana.

Wapinaji hao walishambulia kambi ya Waethiopia katika jengo la wizara ya ulinzi ya zamani ambapo walifyatuwa makombora kwa mizinga pamoja na bunduki za rashasha na Waethiopia wakajibu mapigo kwa kutumia mizinga ya kutungulia ndege.

Miongoni mwa waliouwawa ni watoto ambao walipigwa na makombora na risasi yaliokwenda kombo.

Wiki hii Somalia imeshuhudia mapigano makali kabisa tokea vikosi vya Ethiopia vikisaidiana na wapiganaji wa serikali kuutimuwa muungano wa mahkama za Kislam kutoka Mogadishu mwishoni mwa mwaka jana.Maelfu ya watu hivi sasa wamekuwa wakiukimbia mji mkuu huo.

Nchi hiyo iliokumbwa na umwagaji damu inasubiri kuwekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani 8,000 wa Umoja wa Afrika walioidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo Jumanne.