1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Mapigano yazuka tena.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZe

Watu watano wameuwawa na wengine 10 wamejeruhiwa katika ghasia za hivi karibuni kabisa kuwahi kuukumba mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Polisi na watu walioshuhudia wamesema watu watatu waliuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa leo Jumatatu wakati bomu lilipolipuka karibu na gari baada ya kukosa mahali lilipokusudiwa.

Wapiganaji walivamia kituo cha polisi katika eneo la kusini mwa mji huo mkuu la Holwadag usiku, na kuzusha mapigano ambayo yalisababisha kifo cha kijana mmoja na kuwajeruhi maafisa wawili wa polisi. Majeshi ya Ethiopia na majeshi ya kulinda amani ya umoja wa Afrika kutoka Uganda kwa hivi sasa yanajaribu kuimarisha juhudi za serikali za kuleta amani katika mji wa Mogadishu na kwingineko nchini humo.

Wakati huo huo kazi ya waandishi wa habari imekuwa ngumu katika taifa hilo la Somalia lililokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda wa miaka 16 sasa.