1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Mapigano yazuka tena.

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx7

Milipuko miwili pamoja na mapigano yaliyodumu kwa muda mrefu yamelitikisa eneo la kaskazini ya mji mkuu Mogadishu usiku wa jana , na kusababisha watu wawili kuuwawa , wakati polisi waliwauwa watu wengine wawili wanaosadikiwa kuwa walikuwa waporaji.

Maafisa wa serikali wamekataa kusema lolote kuhusiana na milipuko iliyosikika usiku kucha pamoja na milio ya bunduki katika mji huo mkuu wa Somalia, lakini watu walioshuhudia wamesema kuwa mlipuko mmoja unaonekana kuwa umesababishwa na wapiganaji wakati waliporusha mlipuko huo dhidi ya kituo cha polisi katika wilaya ya Huriwaa.

Hakuna afisa wa polisi aliyeripotiwa kujeruhiwa. Mlipuko mwingine umeripotiwa kutokea katika kituo cha kijeshi cha jeshi la Ethiopia na kusababisha mapigano ya muda mrefu, lakini haikufahamika nani anapigana na nani.