1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mashambulio ya mabomu yauwa watu kadhaa

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBep

Takriban watu watano wameuwawa kufuatia mashambulio mawili tafauti ya mabomu katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

Katika shambulio la kwanza mtu aliyekuwa na bunduki alirusha kombora la mkononi dhidi ya mkahawa mmoja katika kijiji cha Hurwa kusini mwa Mogadishu, watu watatu wameuwawa na wengine watano wamejeruhiwa.

Kwenye shambulio la pili watu wawili wameuwawa kufuataia shambulio la bomu la kutegwa ardhini dhidi ya msafara wa magari ya kijeshi, watu wengine watatu wamejeruhiwa.

Mji mkuu wa Mogadishu umeshuhudia ongezeko la machafuko tangu wapiganaji wanaounga mkono mahakama za kislamu walipoondolewa na majeshi ya serikali ya mpito yakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia.