1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Mazungumzo ya amani kuanza tena

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCu3

Uongozi wa mahkama za Kiislam nchini Somali na wabunge wa serikali ya mpito nchini humo wakiwa katika harakati za dakika ya mwisho kuiepusha nchi hiyo na vita wamekubaliana hapo jana kuanza tena mazungumzo ya amani yanayoongozwa na Umoja wa Waarabu ambayo yalisambaratika mwezi uliopita.

Makubaliano yaliosainiwa na pande hizo mbili yamesema baada ya kukutana wiki hii maafisa wa uongozi wa Kiislam na wabunge wa Somali wakiongozwa na Spika Sharif Sheikh Adan wamekubali kusitisha uhasimu uliopo hivi sasa na kuepuka hatua zozote zile ambazo zitaongeza mivutano.

Lakini haiko wazi iwapo Rais Abdullahi Yusuf na Waziri Mkuu Ali Mohamed Gedi wataridhia makubaliano hayo maafisa wa serikali yao ya mpito hawakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia taarifa hiyo.

Adan anatazamiwa kuwasilisha makubaliano hayo kwa Rais Yusuf kwa lengo la kuidhinishwa kwa kupigiwa kura bungeni.