1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Mkutano wa amani kumalizika leo

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUU

Mkutano wa usuluhishi wa Somalia wenye lengo la kukomesha vita vya miaka 16 na kuhudhuriwa na maelfu ya wajumbe unatazamiwa kumalizika leo hii baada ya wiki sita za mazungumzo ambayo yalitiwa dosari na umwagaji damu wa mara kwa mara mjini Mogadishu.

Kiongozi wa kikabila Bile Mohamud Qabowsade amesema hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wengi kiasi hicho wa Somali kkunga mkono amani na kwa ajili hiyo tu mkutano huo ni msingi wa wa umoja wao wa kipindi cha usoni.

Zaidi ya wajumbe 1,000 wanaowakilisha koo kuu na nyengine ndogo kutoka nchi hiyo ya Pembe ya Afrika wamekutana kwenye mji mkuu huo tete kujadili kushirikiana madaraka na utajiri wa nchi halikadhalika masuala mengine muhimu.