1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Msako mkubwa wa silaha

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJk

Wanajeshi wa Somalia kwa kushirikliana na wale wa Ethiopia leo hii wameingia kwenye soko kuu la Mogadishu kusaka silaha katika jaribio la kukomesha uasi katika mji mkuu huo.

Msako huo wa nyumba hadi nyumba unakuja ikiwa ni siku moja baada ya serikali kufunga soko hilo kubwa la Bakar linaloaminika kuwa ni maficho ya waasi wa itikadi kali za Kiislam ambao wamekuwa wakishambulia mfululizo maeneo ya seikali.

Kwa mujibu wa makadirio watu 60 wengi wao wakiwa ni raia wameuwawa tokea Alhamisi katika mapambano makali kabisa mjini Mogadishu kuwahi kushuhudiwa tokea mwezi wa April wakati vikosi vya Ethiopia vilipowatimuwa wapiganaji wa itikadi kali za Kiislam mjini humo.