1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu: Ndege ya kivita ya Marekani imewashambulia wanaharakati wa mtandao wa al-Qaida huko Somalia.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHd

Ripoti kutoka Somalia zinasema ndege ya kijeshi ya Kimarekani imewashambulia wanaharakati wa mtandao wa al-Qaida ambao wanashukiwa wamehusika katika mashambulio ya mabomu yaliofanyiwa balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania. Vyombo vya habari vya Marekani vinasema ndege hiyo ya chapa AC-130, ikiruka kutokea Jibuti, ilifanya hujuma hiyo huko Kusini mwa Somalia baada ya duru za kijasusi za Kimarekani, zikitumia ndege ya kijasusi isiokuwa na mtu ndani yake, kuwaona wanaharakti hao. Mmoja kati ya watu waliolengwa inaaminiwa ni kiongozi wa cheo cha juu wa mtandao wa al-Qaida katika Afrika Mashariki. Msemaji wa serekali ya Somalia aliliambia shirika la habari la Kifaransa, AFP, kwamba watu wengi waliuwawa katika kijiji cha Badel. Duru ilionukuliwa na shirika la habari la Reuters ilisema shambulio hilo lilifanyiwa kijiji cha Hayo kilioko Kusini mwa Somalia.