1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Ndege ya mizigo yaungua wakati wa kutua

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKs

Ndege ya kubeba mizigo ya Uganda iliyokuwa imebeba vifaa na wanajeshi sita wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, iliwaka moto wakati ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Mogadishu.

Kilichosababisha moto huo hakijajulikana na hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda, amethibitisha kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba vifaa vya kijeshi na wanajeshi hao sita lakini hakuna hasara yoyote iliyosababishwa na moto huo. Aidha Paddy Ankunda amesema anaamini moto huo ulisababishwa na matatizo ya kiufundi.

Walioshuhudia wanasema ndege hiyo iliharibiwa na moto huo. Wazima moto waliuzima moto huo wakisaidiwa na wanajeshi waliokuwa ndani ya ndege hiyo.