1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Polisi ameuawa katika shambulio la waasi

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqP
Polisi mmoja ameuawa na watu waliobeba silaha katika wimbi la mashambulio yanayofanywa dhidi ya vituo vya serikali katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.Polisi wengine 3 pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo.Kwa mujibu wa afisa wa polisi,waasi waliokuwa na silaha kubwa walishambulia kituo cha polisi wakati wa usiku katika mtaa wa Huriwa,kaskazini mwa Mogadishu.