1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Raia wanazidi kuukimbia mji mkuu wa Somalia

31 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCDq

Mapigano makali yameendelea katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu kwa siku ya tatu kwa mfululuizo.Kwa mujibu wa Ethiopia,wanajeshi wake pamoja na vikosi vya serikali ya Somalia,wamewaua zaidi ya waasi 200 wa itikadi kali za Kiislamu.Lakini raia wanasema,mji mkuu Mogadishu unashambuliwa kiholela huku hospitali katika mji huo zikizidi kupokea wakazi waliojeruhiwa.Siku ya Ijumaa,waasi waliangusha helikopta ya jeshi la Kiethiopia mjini Mogadishu.Halmashauri ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi duniani, inatathmini kuwa katika juma lililopita peke yake,kama watu 12,000 wameukimbia mji mkuu.Kwa hivyo,tangu mwezi wa Februari idadi ya wakimbizi imefikia 57,000.