1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Somalia yasema imedhibiti maeneo yote yaliokuwa yakisimamiwa na wanamgambo wa Kiislamu.

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdd

Serikali ya mpito ya Somalia imesema imechukua udhibiti wa maeneo yote yaliyokuwa yakisimamiwa na wanamgambo wa Kiislamu.

Waziri Mkuu, Ali Mohamed Gedi, amesema hatarajii mapigano makali kutokea tena kati ya majeshi ya serikali na wanamgambo wa Kiislamu.

Ali Mohamed Gedi amewataka raia wa Somalia kusalimisha silaha walizo nazo.

Ethiopia, ambayo iliisaidia kijeshi serikali ya Somalia, imesema itachukua muda wa wiki kadhaa kuisaidia serikali hiyo kudhibiti hali nchini humo.

Hata hivyo, mapigano yaliarifiwa kutokea, ambapo ndege za Ethiopia zilizokuwa zikiwaandama wanamgambo wa Kiislamu zilirusha mabomu kwa makosa katika vijiji vilivyo karibu na mpaka kwenye ardhi ya Kenya.

Maafisa wa serikali ya Kenya wamesema wamewakamata kiasi raia wanane wa kigeni wanaoshukiwa walikuwa wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu nchini Somalia.