1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Vikosi vya amani kupelekwa Somalia

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCa9

Vikosi vya amani vya mwanzo vya Umoja wa Afrika, vinatazamiwa kupelekwa Somalia mwezi huu.Taarifa hiyo imethibitishwa na mfanyakazi wa ngazi ya juu katika Umoja wa Afrika.Kuambatana na mpango huo,Uganda itapeleka kikosi cha kwanza.Wakati huo huo waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia, Ali Ghedi kutoka mjini Baidoa ameongezea kuwa Umoja wa Afrika umearifiwa pia na Afrika Kusini,Nigeria,Malawi na Senegal kuwa zipo tayari kupeleka wanajeshi wao.Kwa upande mwingine, stesheni tatu za redio pamoja na ofisi za stesheni ya televisheni ya Kiarabu-Al Jazeera zilizofungwa na serikali ya mpito hapo awali,sasa zinaruhusiwa kuendelea kufanya kazi nchini Somalia.Amri ya kuzifunga ofísi hizo ilizusha upinzani mkubwa.Vyombo hivyo vya habari vimelaumiwa na serikali kuwa vilichochea machafuko na viliwaunga mkono wanamgambo wa Kiislamu waliotimuliwa.