1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Vikosi vya serikali vyaingia Mogadishu

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfL

Vikosi vya serikali ya Somalia vikungwa mkono na vile vya Ethiopia vimeingia kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu baada ya vikosi vya wapiganaji wa Kiislam kuutelekeza mji huo na kukimbia.

Hata hivyo imeelezwa kwamba ni vikosi vya serikali tu ndio vilivyoingia kwenye mji huo na kwamba vile vya Ethiopia vimebakia kwenye viunga vya mji huo.Awali serikali ya Somalia ilitangaza hali ya hatari nchini kote na kusema kwamba kipau mbele chakecha kwanza itakuwa ni kurudisha utulivu na utawala wa sheria.

Kuanguka kwa mji wa Mogadishu kumekuja siku 10 baada ya wapiganaji wa Kiislam kutaka kuvamia makao makuu ya serikali ya mpito yalioko katika mji wa Baidoa.Jambo hilo limeifanya Ethiopia iingie vitani moja kwa moja kuinusuru serikali hiyo ya mpito ilio dhaifu na kuwatimuwa wapiganaji wa Kiislam.

Wakati huo huo uongozi wa Kiislam umekiri kujitiowa Mogadishu lakini umeapa kuanzisha vita vya chini kwa chini dhidi ya serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.